Daktari wa usapuaji nchini Afrika Kusini amethibitisha
kwamba mwanamme wa kwanza aliyepandikizwa uume atakuwa baba hivi karibuni.
Professor
Andre van der Merwe, ambaye ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba,
ameiambia BBC kwamba mwenza wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi minne.
Mwanamme
huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anapashwa
tohara ambayo haikufanikiwa.
Professor
van der Merwe ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa upandikizwaji huo
wa kiungo umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa wagonjwa wengine katika siku
zijazo.
No comments:
Post a Comment