MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM)
amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na
shinikizo la damu kwa muda mrefu.
Taarifa
iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
kwamba marehemu alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu na
amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.
Ameongeza
kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli
ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Shughuli
ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni ya 152 kuahirisha
bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.
GPL
No comments:
Post a Comment