Waziri wa fedha, Saada Mkuya |
Serikali imesema kuwa inafanya utaratibu wa kuwalipa
fedha takribani Sh. bilioni 19 za waliokuwa wanachama wa Taasisi ya Development
Entrepreneurship Community Initiative (Deci).
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Waziri wa Fedha,
Saada Mkuya, alisema fedha hizo zimehifadhiwa katika akaunti ya Benki Kuu (BoT)
na kwamba kinachofanyika sasa ni uangalizi wa kiasi cha michango iliyochangwa
na wanachama ili waweze kulipwa kwa usahihi.
“Bado fedha zinashikiliwa BoT uchambuzi unaendelea
kufanywa kwa umakini wa hali ya juu, utakapokamilika wanachama wote waliochanga
fedha watalipwa,” alisema Mkuya.
Aidha, Waziri Mkuya alisema siyo jambo litakaloweza
kuchukua muda mfupi kukamilisha mchakato wa malipo ya wanachama hao, kwani
linahitaji muda wa kutosha kufanyiwa kazi kikamilifu, ingawa hakutaja kiasi
kilichopo.
Mwaka 2009 serikali ilisitisha shughuli za Deci na
kuwafungulia mashtaka wakurugenzi watano wa taasisi hiyo katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na Agosti 19, mwaka 2013, walihukumiwa.
No comments:
Post a Comment