Tuesday, January 27, 2015

Kama haya ni ya kweli huyu mama inabidi apimwe akili maskini, watoto wavyolia kweli wa kwanza na wa pili!!

    Mama aua watoto wake wawili kwa kuwanyonga 

JESHI la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mwanamke aliyetajwa kwa jina la Zuhura Sudi (26) kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wawili kwa kuwakaba shingo hadi kufa kisha kuwafunga kwenye sandarusi na kuwazika ndani ya nyumba yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Mtaa wa Bakari, Kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora.

Kamanda alisema, Zuhura anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kuua watoto wake wawili Mwamvua Mrisho (miaka 4) na Sudi Mrisho (miezi minne).

"Mtuhumiwa aliwakaba shingoni hadi kufa kisha aliwafunga kwenye sandarusi na kuwafukia katika mashimo mawili tofauti aliyochimba ndani ya nyumba anayoishi," alisema Kamanda Kaganda.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani. Alisema Jeshi la Polisi linalaani vikali kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo.

No comments:

Post a Comment