Wednesday, January 28, 2015

Jinsi ya kuendelea kuwa na morali wakati wa kusafisha


Kwanza kabisa acha niseme kuwa roughly asilimia zaidi ya 90 ya watu kusafisha sio kazi ya burudani. Lakini ukweli ni kwamba, inatakiwa kusafisha kila siku katika maisha yetu, kwa ajili itaboresha maisha yako. Kwahivyo nikiwa nimeshasema hayo, ni muhimu kutopoteza mwelekeo.

Kwangu mimi moja ya kiburudisho kinachoniongezea morali wakati wa kusafisha ni mziki. Nasikiliza mziki wangu huku nafagia, na kinachofuata ni nini ujue? Mtu anashangaa nacheza huku nimeshika ufagio. Kusema kweli inaleta mabadiliko. Ulishawahi kuosha vyombo sehemu ipo kimyaaa, inaboa, unasafisha huku unawaza nitamaliza saa ngapi. Kwanini usiweke kiredio japo kidogo jikoni? Unaosha vyombo huku unakula mziki taratibu, mara unashtukia umemaliza.

Asante kwa kusoma na tutakutana kwenye tip nyingine.


No comments:

Post a Comment