Friday, January 30, 2015

FROM ME: Kanuni kuu 3 za kusafisha ndani ya nyumba sakafu ya kusafishwa kwa maji


  • Ainisha maeneo ya kusafisha .Hii inasaidia hata unapokuwa na mtu wa kukufanyia usafi anakuwa anafahamu mwisho wa usafi wake.
  • Hakikisha una zana  na vifaa vinavyotakiwa kwa ajili ya kusafishia, kwa uchache kama unasafisha ndani eneo ambalo ni la kudeki (halina carpet) unatakiwa kuwa na malighafi za kitambaa za aina tatu. Kitambaa cha kwanza ni taulo au mop kwa ajili ya kudekia, cha pili ni kitaulo kilicholoa kwa ajili ya kufutia maeneo yanayopaswa kufutwa kwa maji na cha tatu ni kitaulo kikavu kwa ajili ya kufutia maeneo yasiyopaswa kufutwa kwa maji kama kwenye vioo. Kwa maeneo mengine mengi kitaulo kilicholoa kinafaa zaidi kwa kuwa kwangu mimi sioni kama kikavu kinafanya kazi effective. Mwishoni utahitaji maji, sabuni, all-purpose au glass cleaner au windex. Vifaa hivi vinakupasa kuwa mkononi kwa usafi wa ndani kusikokuwa na carpet.
  • Safisha kuanzia juu kwenda chini na kwa kufuta peleka mkono clockwise (kama saa inavyotembea) na safisha kuelekea nje. Kwa njia hii hutakuwa na vumbi linaloanguka tena juu ya sakafu yako ambayo umeshasafisha.
Unaonaje uka print ukampa dada wa kazi ajifunze kanuni hizi ili akurahisishie kazi ya kuelekeza kila wakati?

No comments:

Post a Comment