Wednesday, January 28, 2015

Suluhisho la vifaa vya kuhifadhia kwenye sebule za kisasa

Eneo la kutosha la kuhifadhia kwa wamiliki wengi wa mijengo ni issue hasa pale familia inapoanza kukua, na ni tatizo hasa sebuleni. Kama tunavyojua sebule (zilizo nyingi) hazina closet au stoo lakini ni mahali ambapo familia nyingi zinatumia muda mwingi zaidi . DVD, matoy, game na vitabu ni baadhi ya vitu  vinavyotakiwa kuwa karibu pale mnapokuwa kama famili pamoja sebuleni mki enjoy family time. Kuwa na sehemu ya kuhifadhi vitu hivi vya ziada inaweza kuwa changamoto.


Suluhisho hili la kuhifadhi linaweza kuwa la kisasa zaidi na kuoana kabisa na muonekano wako wa sebule. Hizi ni vitu vinaitwa ottomans, na kwa vile vina matumizi zaidi ya moja, ni sahihi hata kwa sebule ndogo.
Zaidi ya kuongeza eneo la kuhifadhia vitu vidogodogo, ni rahisi kukisogeza na mgeni aliyezidi akakalia. 
Nilishatembela nyumba moja nikakutana na kama hiki, kina zipu kwa chini (huwezi kuiona kikiwa kimekaa kama hivi). Wenyeji walikuwa wanahifadhia nguo zilizowaruka watoto zikisubiri kuwa donated na wenyewe walikuwa wanakiita benki ya nguo. Kikaptula cha mtoto kikimruka unasikia kiweke kwenye benki ya nguo. Wakati huohuo mtu anakikalia sebuleni. So nice...
Pia unaweza ukaweka trei juu yake kutengeneza eneo flat ukasevu vitafunwa au vinywaji au kadi za kuchezea karata.

No comments:

Post a Comment