Monday, January 26, 2015

Jinsi ya kuhamasika kusafisha



Kuhamasika kusafisha sio kitu rahisi eti. Baada ya ku practice kwa miaka mingi nimeweza kupata dondoo bomba za kukuhamasha kusafisha. Hapa ni tatu ninazozipenda zaidi:
 
Safisha asubuhi – Anza siku yako kwa kuweka mazingira safi ili uweze kuifurahia siku iliyobaki. Anza na ule usafi mgumu ili kukufanya usirudi kitandani.
 
Tenga muda wa kusafisha- Weka muda mchache pembeni kila siku kwa ajili ya kusafisha.
 
Epuka distractions wakati wa kusafisha- Kwa mfano zima simu na usikatize hadi umalize usafi wako, labda iwe ni kwa jambo muhimu sana. Usideki nusu ukasema ngojea ninywe chai kwanza.

No comments:

Post a Comment