Tuesday, January 27, 2015

Interesting: Wanawake na wanaume wanapogombana twitter


Maelfu ya wanaume nchini Saudia wanajaribu kuwatoa wanawake katika mtandao wa twitter ,lakini juhudi hizo zinaonekana kuambulia patupu.

Ukandamizaji wa kijinsia nchini Saudi Arabia ni swala la kawaida na inaonekana baadhi ya watu wanajaribu kulipanua wazo hilo kufika katika mitandao ya kijamii.
Maneno yaliosema ''hatutaki wasichana katika mtandao wa Twitter'' yalitajwa takriban mara 400,000 wikendi iliopita.

Hata hivyo chimbuko la maeneo hayo halijulikani.
Lakini ajenda ya wazo hilo haikufanikiwa kwa kuwa wengi waliojiunga walikuwa wakipinga ukandamizaji huo wa kijinsia.
Wanawake walijibu nao kwa kusema ''kwa nini? Tumefanya nini''? .
Mwingine aliandika kwa kusema ''iwapo kungekuwa hakuna wasichana katika Twitter hakuna mwanamume ambaye angejisajili''.

Wanawake wengine pia walianza kusambaza ujumbe uliosema ''hatutaki wanaume katika twitter'', ili kulipiza kisasi lakini ilipata ujumbe 1,500 pekee.

No comments:

Post a Comment