MCHUMI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Brown Kajange (42) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo
kujibu mashitaka mawili, likiwamo la shambulio la aibu kwa kumshika matiti
mwanamke bila ridhaa yake.
Shao alidai siku ya tukio saa 6 mchana katika eneo
hilo, mshtakiwa alimshika matiti Queensia Fusi bila ridhaa yake huku akijua
kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Alidai kuwa shtaka la pili, mshtakiwa alimpiga
ngumi mlalamikaji katika jicho la kushoto na kusababisha maumivu makali katika
sehemu hiyo. Mshtakiwa alikana mashtaka na Hakimu Luanda aliahirisha kesi hiyo
hadi Machi 3, mwaka huu itakapotajwa.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza
masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka serikali ya
mtaa, atakayesaini bondi ya Sh 300,000. Chanzo Habari Leo
No comments:
Post a Comment