Shule zote za serikali zikiwemo za
msingi na zile za upili nchini Uingereza zitalazimika kufunza somo la ngono na
uhusiano SRE ,wabunge wa taifa hilo wamesema katika ripoti yao.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham
Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata habari ambazo
zitahakikisha usalama wao.
Serikali imesema kuwa itaangazia
matokeo ya ripoti hiyo.
Mwaka 2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii ,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule.
Wabunge hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini.
CHANZO:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment