Hii miaka itakuacha ucheke na maandishi..
Mahakama ya Afrika Kusini imemfunga jela miaka 1,535
mwanaume mwenye umri wa miaka 35 ambaye alibaka wanawake katika kipindi
cha miaka mitano, vyombo vya habari viliripoti jana.
Kwa mujibu wa mtandao wa deccanchronicle jana, uhalifu
huo wa jamaa huyo Albert Morake wa eneo la Tembisa katika Jimbo la Gauteng
ulianza mwaka 2007 na kukoma mwaka 2012 wakati alipokamatwa na polisi.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 1,535 jela na Mahakama ya
Juu ya Johannesburg kutokana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya jela miaka
30 kwa matukio 30 ya ubakaji, miaka 360 jela kwa matukio ya uporaji na miaka
mingine mia kadhaa kwa mashtaka mengine zaidi ikiwemo kujaribu kuua, kuteka
watu na ukabaji.
Vyombo vya habari vilisema kuwa, Morake ni mmoja wa watu
waliofanya matukio ya ubakaji mabaya mfululizo nchini Afrika Kusini na kifungo
dhidi yake ni moja ya vifungo adimu.
Watu waliowahi kubakwa, waliohudhuria sehemu ya adhabu
aliyopewa mshtakiwa, walicheza kwa furaha na kukumbatiana kila mmoja.
Morake alikanusha mashtaka 175, ikiwemo kubaka watu 30,
kuteka watu 41 na kukaba watu wengine 24.
Hata hivyo, alipatikana na hatia katika makosa 144.
Hukumu hizo atazitumikia kwa wakati mmoa.
Jaji Rean Strydom alisema kuwa, Morake hakuonesha
masikitiko na aliendelea kukanusha kuhusishwa katika matukio hayo ya uhalifu.
"Alikuwa mjinga kwa kuwashauri aliowatendea uhalifu
jinsi ya kujilinda dhidi ya kubakwa siku zijazo," alinukuliwa jaji huyo
akisema. Strydom alisema, wengi wa wahanga wa Morake walifanyiwa uhalifu kwa
kushtukizwa na walishikwa mihemko wakati walipokuwa wakitoa ushahidi dhidi
yake.
No comments:
Post a Comment