Interest yangu kwenye hii picha sio hiyo blackboard bali ni hii stand ya viatu. Imagine una watoto watatu wadogo nyumbani ambao hawajafikisha umri wa miaka 15, jinsi ambavyo viatu ndani vinakuwa vingi. Ukiwa na stand kama hii unakuwa umeaga shida ya sehemu ya kuhifadhi viatu vyao.
Na uzuri wa stand ya mfano huu inaweza kuwa imezibwa nyuma au inapata support ya ukuta, lakini kikubwa zaidi ni hivi vibox kila pair ya kiatu kuwa kwenye kibox chake!
Kuna zile stand ambazo hazijagawanywa hivi na changamoto yake ni kuwa unachukua kiatu kimoja halafu kadhaa vinadondoka (na unajua viatu vya watoto wadogo ni vidogodogo) basi ni kadhia ya kuanza kupanga tena upya.
Since hii ni mbao inaweza kuwa ghali lakini ukitengeneza kama hii ni suluhisho la kuhifadhi viatu vya wanao miaka nenda rudi hadi watakapokuaga kwenda kujitegemea. Halafu stand inatulia kusubiri wajukuu wakija kukutembelea. Eeh hautaishi na watoto wako siku zote, hata kuku anafukuza vifaranga vyake vikishakua sembuse binadamu.
No comments:
Post a Comment