Wanawake wa Uturuki sasa wameamua kuuvunja ukimya na
kuzungumzia masuala ya ubakaji,unyanyasaji wa kinsia,na unyanyasaji kwa
ujumla.BBC nchini Uturuki ilimuuliza Profesa maarufu nchini humo Sahika Yuksel,
ni kwa namna gani akili ya mbakaji inavyofanya kazi.
Maandamano makuba yaliratibiwa na kusambaa kote nchini
humo mwishoni mwa wiki wakitumia jina la binti aliyeuawa na lilitumika kwenye
mitandao ya kijamii mara 3,300,000. Na zaidi ya hapo katika mitandao ya kijamii
wanawake wengine pia waliibuka na majina ya wanawake waliohusika katika
unyanyasaji wa kijinsia na kueleza kilichowakuta.
Kwanini wanaume wanabaka? Nini kinachosababisha ubakaji? Kwanini
wanaume wanabaka?
Ni makosa makubwa kukisia kuwa wanaume wanabaka kutokana
na matamanio ya miili yao. Mbona mwanamume aliyeko mtaani hawezi kumbaka
mwanamke mpita njia kwa namna hiyo.pamoja na kutambua kwamba haifai,huthubutu
kutekeleza ubakaji kwa usiri mkubwa ,mbali na macho ya watu.
Ubakaji si tendo la ndoa. Ubakaji ni shambulio, ni suala
la nani mshindi, ni kama umeshikilia kitu na mwanamke ndiye mlengwa katika
suala hili ni sula la mmoja mwenye nguvu ndiye anakuwa mshindi na wapo baadhi
ya watu wanaopata faraja kutokana na ubakaji.
Ubakaji sio kosa pekee ambalo mwanaume huwa
anafanya.Shambulio la mwili,mwili kudhuriwa ,kupuuzia haki za wanawake,na
udhalilishaji ubakaji hutokea mara..
Raha hupotea ikiwa wewe utageuka kuwa muwindwa
Swali:je malezi ndiyo huzalisha mbakaji siku za usoni?
Watoto hukua katika mazingira ya kutakiwa kuwaheshimu
wanaume na utamaduni wa kuonekana wanaume wana mamlaka zaidi ya jinsi
ingine.mwanamke anatakiwa kumhudumia mumewe kwa namna tofauti zaidi na kutakiwa
kutii mamlaka na utawala wa kimabavu wa mwanaume .
Na hapo ndipo mama husafirisha mtazamo na tabia hizo za
kimfumo dume kwa watoto wa kike na wa kiume ,ni wazi kuwa mabinti wanaokulia
katika familia zenye unyanyasaji wa kijinsia,hukumbana na unyanyasaji mkubwa zaidi
katika ndoa zao ama katika mahusiano yao.
Wanaume walioshuhudia mama zao wakipigwa na baba zao wao
pia huwa na tabia ya unyanyasaji katika mahusiano yao.wasicha na wavulana
hutambulika katika jamii kwa namna mama zao walivyotendewa na baba zao na hiyo
ndio sababu ya msingi.
Unaweza kusema kuwa hili ni tatizo la ulimwengu na
unaweza kushuhudia matukio yenye sifa za kufanana ulimwenguni kote.lakini
utofauti huonekana wakati wa kushughulikia ama kupambana na suala hili.wanawake
nchini Uturuki huwa hawapati elimu ya kutosha kama ambavyo wanaume wanavyopewa
kipamumbele.Nao wanasiasa wamemaliza mzizi wa fitna na kuweka ubaguzi bayana
kwa kudai kuwa wanawake na waume hawawiani.
Ukinzani shurti utokee kwa tabia chafu
swali:Unawezaje kujihusisha na mwanaume mwenye mtazamo na
tabia za namna hiyo na mhitaji?
Hakuna atakaye weza kuibadili kama hatang’amua na
kukubali kuwa tabia zake ni mbaya na kuwajibika kwazo.kama atakamatwa na kukiri
kuwa hakumaanisha kutenda hayo hii haitaleta mabadiliko ya tabia.
Idadi ya wanaume wanaogundua tabia zao zisizofaa zenye
kuathiri jinsi ingine na kuhitaji msaada kabla hawakamatwa ni ndogo mno.
Namna pekee ya kukabiliana na tabia za namna hii ni
kuwaweka katika vituo vya mabadiliko ya tabia wanaume wenye tabia za nman hii
wakati wakitumikia vifungo vyao.Njia hii haitumiki sana nchini Uturuki .kila
mmoja ana haki ya kuhudumiwa na kutafutiwa tiba ya tatizo lake.
Vipo vituo vingi vinavyoshughulika na mabadiliko ya tabia
kwa wabakaji ulimwenguni ,na matukio ya kushambuliana wao kwa wao ni machache
mno ukilinganisha na wale wasiopatiwa huduma hiyo jela.mpango huu wa tiba ni
maalumu kwa vijana waliobalehe na wenye tabia za unyanyasaji wa jinsia .
Ningependa kugusia suala moja katika mazungumzo haya
.Kuna haja ya kuwahasi wanaume wabakaji lakini nadhani adhabu ya kifo
inahitajika tena.Lakini adhabu ya kifo si kibinadamu, sote tunajua ya kwamba
nchini Marekani ,matukio ya uhalifu si ya kiwango cha chini katika nchi ambayo
adhabu ya kifo inatekelezwa.
Hatua hii ya adhabu ya kifo sio kipimo tosha cha
kukomesha uhalifu.watu walio katika nafasi za juu za uongozi hujaribu kutuliza
jamii za watu.na mara zote maandamano na kelele hizi husikika mara tu matukio
ya ubakaji yanapotukia,hatuzungumzii suala la ulipizaji wa kisasi hapa.lengo
letu ni kwa jamii zetu kuwa huru na unyanyasaji wa kingono na ubakaji kadiri
inavyowezekana.
Vunja ukimya.
swali: Mwanamke wa umri wowote aliyebakwa afanye
nini,kama atakuwa jasiri wa kusema kuwa kabakwa.
Katika jamii na tamaduni zetu ambako suala la ngono
limefanywa kuwa suala la kawaida na ndoa za utotoni ama za mapema naweza kusema
zinapingwa, mashambulio ya kingono huwa ni nadra kutukia.
Mbakaji analijua hili fika lakini humtisha mwanamke
anayembaka kuwa ataifahamisha familia ya mwanamke huyo kilichotokea na
huendelea kutenda kosa hilo lililo kinyume cha utu.na wakati mwingine humgeuka
mwanamke anaymbaka na kuwaeleza marafiki zake juu ya mwanamke huyo kwa matukio
mengine zaidi ya ubakaji.
Mwanamke aliyebakwa anaweza kuchukua hatua za
kisheria,anaweza pia kupata msaada wa kisaikolojia na uungwaji mkono na jamii.
Lakini pia anaweza kuongea na marafiki zake wa karibu anaowaamini.Na hii ndio
njia pekee ya kupata uponyaji ama nafuu ya matukio ya mashambulio ya kingono
ama unyanyasaji na usikae kimya juu ya masuala ya namna hiyo.
jamii ikiwa pamoja huleta ahueni
Mashambulizi ya kingono yanaweza kuleta matatizo ya
kiafya,magonjwa ya kuambukiza na hata ujauzito.zaidi ya hayo mwananke
aliyebakwa anapaswa kuchunguzwa haraka iwezekanavyo na hatua za haraka hazina
budi kuchukuliwa dhidi yake kiafya.
Inawezekana kukawa na matatizo ya muda mfupi ama ya muda
mrefu ambayo yanahitaji huduma baada ya ubakaji kutokea.lakini pia kuna haja ya
kuwa na vituo vya kuhudumia watu waliokumbana na unyanyasaji wa kijinsia,mahala
ambapo msaada stahiki unapatikana na kutolewa mara moja bila kukawia.
Pia mwanamume ambaye mpenzi wake amekumbwa na unyanyasaji
wa kijinsia hana budi kuwa na mpenziwe katika kipindi hicho kigumu na wakati
huo huo akipokea matibabu ya kisaikolojia na msaada wa kijamii pia.
No comments:
Post a Comment