Solar panel ikifungwa juu ya paa |
Benard ni mmliki wa kampuni ya vifaa vya kufunga umeme wa
jua kwenye majengo ya makazi na ya biashara. Anasema alichosomea yeye ni
Environmental Science na alipotoka shule aliajiriwa kama sales manager kwenye
kampuni iliyokuwa ikihusika na solar energy. Baada ya miaka sita akaamua
kujiajiri.
Nimemuuliza kwanini aliamua kujiajiri. Akasema ni impact
aliyoona kwa vifaa vya solar walivyokuwa wakifungia wateja wao. Kwa mfano
kubadilisha dispensary ya kijijini iliyokuwa ikitumia kibatari na kufanikiwa
kutumia taa, feni na computer walau moja. Kwake hiyo ilimgusa sana ndipo
akasema naye anataka kuwa na kampuni yake ili aweze kuendelea kusaidia watu kwa
namna hiyo hiyo kwa wingi na uhuru zaidi.
Benard anasema katika kujiajiri unapata kila unachokitaka
kwa muda wako ila mwisho wa mwezi unatoa badala ya kupokea. Yani alipokuwa
ameajiriwa yeye alichokuwa anajua ni kuwa mwisho wa mwezi anapokea, lakini kwa
sasa kuwa na kampuni yake tofauti ni kuwa mwisho wa mwezi anatoa. Na hapo ndipo
penye changamoto kubwa mno anasema. Ukiwa umejiajiri unaweza kulala, kusafiri,
kufanya chochote unachotaka na kwa muda wako bila mtu kukupangia, ila kimbembe
ni mwisho wa mwezi.
Benard anashauri ni vyema mtu anapotoka shule aajiriwe
kwanza kabla ya kujiajiri. Kwanini? Kwa sababu anasema unapojiajiri una manage
watu, sasa kama hukuwa mwenyewe managed inakuwa ngumu kujua ilivyo vigumu
ku manage watu. Watu hawako so pefect kwahivyo wakubali walivyo, anasema.
Benard anasema pamoja na changamoto za hapa na pale
anajivunia zaidi kujiajiri kuliko kuajiriwa, anafunga inveta za kuchaji kwa
umeme na za kuchaji kwa solar, heater za solar za maji ya moto na solar za
majumbani na maofsini. Kwa hivyo hizi inveta za kuchaji kwa umeme ni kwamba umeme unapokuwepo unachaji inveta yako, endapo utakatika unaiwasha, haina kelele na haihitaji system mpya ya waya, inatumia zilezile za umeme wa kawaida, kinachokuwepo ndani ni kiboksi kidogo tu.
inveta na betri yake |
Bei ya hizi solar zina range kuanzia milioni moja na
nusu hadi milioni 20. Kwa mfano anasema mfumo wa solar wa kuweza kuwasha laptop
1, TV 1 na taa 6 gharama yake ni milioni moja na laki nane.
Umehamasika? Usikose “nitavukaje” itakayofuata.
No comments:
Post a Comment