POLISI aliyekuwa
akikabiliwa na kesi ya kumbaka mahabusu katika kituo kidogo cha Ilembula
wilayani Wanging'ombe mkoani hapa, Juma Nyambega, amehukumiwa kifungo cha miaka
30 jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Njombe kuridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo.
Majira linaripoti kuwa:
Askari huyo mweye
namba F 6565 alihukumiwa adhabu hiyo na mahakama ya Wilaya ya Njombe mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi Augustine Rwezile.
Akisoma hukumu
hiyo, Rwezile alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa
upande wa mlalamikaji pamoja na vielelezo vya daktari aliyempima binti huyo
mwenye umri wa miaka 19 na kubaini kuwepo kwa michubuko sehemu zake za siri.
Askari huyo
alipandiswa mahakamani hapo kwa kosa la kumbaka binti huyo, aliyekuwa amewekwa
mahabusu. Ilidaiwa kuwa alitolewa kwenye chumba cha mahabusu na kumbaka.
"Mahakama
baada ya kusikiliza maelezo ya daktari aliyempima binti huyo na maelezo ya
upande wa mlalamikali imebaini kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo na mahakama
inamuhukumu kwenda jela miaka 30,"alisema hakimu huyo.
Alisema mshtakiwa
kama atakuwa hajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama yake
anaruhusiwa kukata rufaa. Awali akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali
Magdalena Kisowa aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 10,
mwaka jana saa 2 usiku akiwa kituo cha polisi.
Siku ya tukio hilo
askari huyo alikwenda kwenye chumba cha mahabusu ambacho alikuwepo mlalamikaji
na kumwambia kwamba anampeleka chumba kingine ambacho kilikuwa na mwanga na
kisha kumbaka.
Aidha wakili Kisowa
aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa
watu wengine wenye tabia kama hizo za ubakaji kwani kitendo hicho ni cha
unyanyasaji na udhalilishaji kwa mwanamke.
No comments:
Post a Comment