Mzazi jitahidi kadri uwezavyo kuhakikisha kuwa kila wakati mwanao yuko kwenye uangalizi, jamani.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani
Tabora imemhukumu kifungo cha maisha Kashindje Shija (50), baada ya kupatikana
na kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitano.
Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Mkazi
wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega Joseph Ngomero, alisema kuwa, kutokana na
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, amelazimika kutoa hukumu hiyo ili iwe
fundisho kwa watu wengine wanaokusudia kufanya vitendo kama hivyo.
Hakimu Ngomero aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana
na kitendo cha kinyama alichokifanya Shija cha kumbaka mtoto mwenye umri wa
miaka 5, mahakama hiyo imelazimika kumhukumu kifungo cha maisha jela.
Awali Mwendesha Mashitaka wa Serikali wilayani
Nzega Melito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa, mnamo Mei 19, 2014 katika
Kijiji cha Kidete wilayani Nzega saa 8 mchana, Shija alifumaniwa chini ya mti
wa mwembe akiwa anambaka mtoto huyo.
Aidha Melito aliongeza kuwa kutokana na kitendo
alichokifanya mtuhumiwa kilimsababishia mtoto huyo maumivu makali katika mwili
wake pamoja na kutoka damu nyingi.
Mwendesha Mashitaka huyo, aliiomba mahakama hiyo
kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kutokana
na kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa cha kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka
5.
ilitoa nafasi ya utetezi kwa mtuhumiwa ambapo
aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu
kutokana na kuwa mwathirika wa virusi vya Ukimwi.
Chanzo: Habari Leo
No comments:
Post a Comment