MSANII wa muziki na mwigizaji wa filamu za Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole’, ameamua kuweka wazi chanzo cha migogoro yake na mumewe
mtarajiwa, Nuh Mziwanda kuwa ni marafiki.
Shilole alidai kuwa mara nyingi wamekuwa wakigombana, lakini chanzo
kikiwa ni maneno ya uchonganishi kutoka kwa marafiki zao wa karibu ambao
wana lengo la kuwatenganisha.
Mwanadada huyo alidai kutokana na hali hiyo, hivi sasa ameamua
kutowahusisha suala lolote linalohusu maisha yake ili kupunguza migogoro
ya mara kwa mara baina yao.
Alisema wale walio karibu yao ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa
kutokea kwa migogoro kwenye mahusiano yao, ukizingatia hivi sasa wapo
kwenye harakati za kufunga ndoa baada ya wazazi wa pande zote kukubali
uhusiano wao.
“Tumegundua kuwa mashoga ndio wanaotugombanisha, kwani kila mara mchumba
wangu anapewa taarifa zinazonihusu mimi huku hao hao wakiniletea habari
zake, jambo hili limesabababisha nisihitaji tena marafiki wengi wao ni
wanafiki,”alisema-Mtanzania
No comments:
Post a Comment