Monday, February 23, 2015

KUTOKA KWANGU: Njia rahisi ya kusafisha kitako cha pasi

Ni kawaida kukuta kitako cha pasi kimeungua na kikichafua nguo nyeupe. Hatua hizi chache zitakusaidia kufanya pasi yako iwe safi tena bila kukwangua layer yake original.
Ni rahisi, unahitaji dakika 20-30 tu, twende kazi:

Hakikisha pasi imechomolewa kwenye umeme na imepoa. Tengeneza uji mzito wa baking soda (nielewe vizuri, nimesema baking soda na sio hamira) kwa kipimo cha kijiko kimoja cha maji (kijiko cha mezani sio cha chai) kwa vijiko viwili vya baking soda vya ukubwa huohuo, koroga changanya kufanya kitu kizito kama dawa ya mswaki.

Paka huu uji kwenye kitako cha pasi kwa kutumia sponji na zingatia kupaka zaidi pale palipoungua. Sugua halafu tumia kitambaa kisafi kuondoa mchanganyiko wote kwenye pasi. Kama ni zile pasi zenye matundu ya maji pitisha kitu/kijiti kuondoa uji uliongia humo.

Washa pasi, chukua kitambaa cha kusafishia cha pamba kinyooshe ili uchafu uondoke kwenye pasi ambapo pamoja na kubonyeza mvuke uchafu uliobakia utatoka. Zima pasi, chukua kitambaa kilicholoa kiasi na malizia kufuta pasi yako kwa mara ya mwisho kuondoa takataka zozote zilizobaki.
   

No comments:

Post a Comment