Sikuwa nafahamu hili..,
GPL inaripoti kuwa: NDOA ya staa wa filamu nchini, Salim Mbegu ‘Slim’ na
mkewe Asia Morgan imevunjwa rasmi na Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni
jijini Dar kufuatia mgogoro wa muda mrefu.
“Mahakama hii imevunja baada ya mdai (mke) kusema hata iweje hawezi
kurudi tena kwa mumewe huyo kutokana na kuwa na wivu wa kupindukia na
kingine kibaya walivyokuwa kwenye mgogoro kuna mwanamke alikuwa
akijinadi kwa kupiga picha nyumbani kwa mumewe na kuzituma kwenye
mtandao wa kijamii wa Instagram,” alisema Hakimu Mwanaidi Madeni wa
mahakama hiyo.
Hakimu aliamuru watalaka hao kugawana mali zote walizochuma pamoja
likiwemo gari walilozawadiwa wakati wa harusi yao, ambalo ndilo lilikuwa
chanzo cha mgogoro huo.Wakati mume akisema anaiheshimu hukumu hiyo
ingawa anaona kama ni filamu, mke alionyesha furaha yake na kudai sasa
ataishi kwa amani.
No comments:
Post a Comment