Ni kama swali la kijinga vile, “kwanini
nitandike kitanda?”
Sababu chache hizi hapa kwa kadri
ninavyoona mimi:
Kitanda kilichovurugika kinafanya
chumba kizima kionekane mvurugano, wakati ambapo kitanda kilichotandikwa
kinafanya chumba kionekane nadhifu hata kama vitu vingine haviko sawa kivile.
Nyumba zetu hizi tunavyozijua, si
ajabu kukuta umelala na mdudu kitandani wakati kitanda
kingekuwa kimetandikwa
ingekuwa rahisi kumuona.
Kutandika kitanda inakupa morali wa
kutoka kwenda kutafuta rizki badala ya kurudi kitandani kulala.
Unaburudika wakati unaporudi
nyumbani na kuingia chumbani kitanda kikiwa kimetandikwa.
Inazuia aibu, nina uhakika huenda
ulishakutana na hili, unaacha nyumba/chumba chako shaghalabagala mara unapata mgeni
ambaye hukumtegemea. Hata ukisema aah, I don’t care…nina uhakika unajisikia aibu fulani hivi ndani ya nafsi.
Kwanini unaosha vyombo? Unaenda
kuvitumia tena, sio? Kwanini unamwaga taka, kwani hutazalisha tena taka baadaye?
Kufanya kitu kimoja kiwe katika hali ya usafi kinakupa hatua nyingine ya
kusonga mbele. Hata kama huwezi kufanya chochote lakini hushindwi kutandika
kitanda chako.
Kutandika kitanda haitakiwi kuwa
ishu, ni kiasi cha kunyoosha shuka, panga mito na tandaza blanketi, basi.
Kwa mawazo yako ni nini faida na
hasara za kutandika kitanda?
No comments:
Post a Comment