Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro, Leonidas Gama. |
Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa ukatili wa kijinsia wa utelekezaji familia kutokana na waume kufukuza wake zao na watoto na kuchangia ongezeko la watoto wa mitaani.
Akizungumza juzi na waandishi katika mafunzo yalioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), kuhusu uandikaji wa matukio ya ukatili wa kijinsia, Inspekta Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia Mkoa huo, Priscal
Maganga, alisema wanaume mkoani humo wanaongoza kutelekeza familia zao bila ya kujali kuwa watakula na kulala wapi.
Priscal alisema katika kipindi cha Januari hadi Februari mwaka huu, wamepokea kesi 20 za waume kutekeleza familia.
“Mbaya zaidi unakuta mama na watoto wanafukuzwa usiku wa manane,
hawajala, hawana pa kukimbilia wanakuja hapa kwetu wakiamini tutawapa
chakula na maradhi na sisi Polisi hatuna fungu hilo, inatubidi tuingie
mfukoni kuchangishana ili kuwasaidia,”alisema.
Hata hivyo alisema kesi hizo zimepungua kutoka kesi 50 walizokuwa
wakipokea kwa mwezi kutokana na elimu wanayotoa kwenye mikusanyiko ya
watu.
Alisema kupungua kwa kesi hiyo kunatokana na elimu wanayotoa kwenye mikusanyiko ya watu ya madhara ya kutelekeza familia.
Priscal alisema kwa upande wa ukatili wa kubaka, wamepokea kesi
tano katika kipindi hicho, tatu za kulawiti na moja ya ukatili dhidi ya
mtoto aliyepigwa na wazazi wake kupita kiasi.
“Kesi hizi za kulawiti na kubaka nyingi zipo shuleni na hasa
Manispaa ya Moshi," alisema na kusisitiza kuwa: " Kunahitajika wazazi
kushirikiana na walimu na dawati kutoa elimu kwa watoto wao kuwaeleza
madhara ya ukatili huo."
Chanzo: Nipashe
No comments:
Post a Comment