Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima. |
Hayo yalisema na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Silima, wakati akizungumza na NIPASHE juu ya kuwapo kwa sheria ya fidia
kwa wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu
ya umeme.
Silima alisema suala la Tanesco kulipa fidia kwa wananchi
waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme ni
jambo gumu ambalo haliwezi kutekelezwa kwa haraka.
Alisema Tanesco ina majukumu mengi ikiwamo la kuhakikisha wananchi
wanapatiwa umeme, hivyo kuliongezea mzigo mwingine ni kutaka kulifilisi.
Aliongeza kuwa mbali na kutokea kwa majanga ya moto mara kwa mara
yanayosababishwa na hitilafu ya umeme, siyo kweli kwamba Tanesco
limehusika moja kwa moja kusababisha majanga hayo.
Alisema sikuh izi kuna watu wanajiunganishia umeme kiholela kwa
kuwatumia watu wa mitaani kuwaunganishia umeme jambo ambalo
linasababisha hitilafu ya umeme na wakati mwingine kusababisha majanga.
Silima alisema kuwa mbali na wananchi kujiunganishia umeme
kiholela, pia wananchi wengi wananunua vifaa vya umeme ambavyo siyo
imara kutokana na kutothibitishwa na Shiria la Viwango Tanzania (TBS).
“Ki ukweli kuhusu Tanesco kuanza kulipa fidia kwa wananchi
waliofikwa na majangwa ya moto kulikosababishwa na hitilafu ya umeme ni
vigumu, kwa sababu hitilafu ya umeme inaweza kusababishwa na vitu
vingi,” alisema Silima.
Alisema kama wananchi wanataka kuwapo kwa sheria hiyo, ni lazima
wadau mabalimbali wakae vikao na kujadili kabla haijapelekwa bungeni
kama muswada na baadaye kuwa sheria.
Silima alisema katika nchi nyingine sheria iyo ipo, kwa mashirika
yao ya umeme kuwalipa wateja wake ikigundulika kuwa uzembe wa shirika la
umeme umesababisha kuungua kwa nyumba.
Hivi karibuni, kumekuwapo na matukio mbalimbali ya nyumba kuungua
kunakosababishwa na hitilafu ya umeme, likiwamo tukio la watu sita wa
familia moja kuteketea kwa moto katika ajali ya moto iliyotokea
Kipunguni jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment