Marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake 2012 |
MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia
jioni hii jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Mmoja wa watoto wa Komba ambaye
aliyejitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na
akasema, huku akilia, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu,
Dar.
Habari zinasema asubuhi ya leo Komba
alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini baadaye akajisikia
vibaya, hivyo akaamua kurudi nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake
ilipoamua kumkimbiza Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari
ikathibitika kuwa alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi
sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Kapteni Komba ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania One Theatre (TOT),
ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi inayokwenda na mtindo wa
Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika kampeni zake wakati wa uchaguzi kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga
kura na kushiriki kupiga live kwenye majukwaa ya kisiasa.
Enzi za uhai wake alitamani
sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa Achimenengule uwe wa kitaifa lakini
ikashindikana, na badala yake Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao
umekuwa kama mtindo wa muziki wetu kwa sababu zifuatazo.
Kwanza, ni mtindo halisi wa
Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao ya Tanzania.
Pili, ndiyo
mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’
wa muziki wetu, wana Njenje, The Kilimanjaro Band.
Baada ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo
huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika
Band, wana mipasho kadhaa na mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango
chake kikubwa cha muziki, Bob Haisa.
Sababu ya tatu ni kwamba mtindo huo
umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi, vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa
kulazimisha bali kwa mapenzi tu ya mashabiki wa muziki wa Tanzania.
Kapteni Komba awali alikuwa mwalimu
wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini na kuwa kiongozi wa kikundi cha
maonesho cha jeshi na baadaye Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi
aachane na jeshi na kujiunga na CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa
mwaka 1992.
“Mzee Mwinyi ndiye aliyenifanya
niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama
kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi
kusema hivyo Kapteni Komba.
Ameshiriki kampenzi za marais Ally
Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye madarakani hivi sasa, Jakaya
Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa
Jimbo la Mbinga Magharibi hadi kifo kinamchukua.
Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa
anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Baada ya kurejea nchini alisema
upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika katika Hospitali ya Apollo, India
na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la
damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
MALI ZAKE ZATISHIWA KUUZWA
Mapema mwezi uliyopita mwaka huu,
mali za Kapteni John Komba zilitangazwa kupigwa mnada kutokana na kushindwa
kulipa deni analodaiwa na Benki ya CRDB.
Mali hizo zilihusisha eneo lenye
ukubwa wa mita za mraba 2,214 lililopo Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, kiwanja
namba 1030 kilichosajiliwa kwa jina la John Damiano Komba na Salome Komba.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa
kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya Uwakili ya Mpoki & Associates
Advocates inayoiwakilisha CRDB ilitangaza kuuza eneo hilo la kibiashara
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, maduka makubwa, benki,
sehemu ya kufanyia mazoezi, hospitali na huduma nyingine za kijamii.
Marehemu Komba ameacha mjane, Bi
Salome, ambaye ni mwalimu kitaalumu na watoto kadhaa. Mungu ailaze roho ya
marehemu mahali pema peponi- ameen!
(Stori: Gladness Mallya/ GPL)
No comments:
Post a Comment