Rais Kikwete akizindua rasmi sera ya elimu ya Taifa Dar es salaam jana. |
Gazeti la Habari leo linaripoti kuwa:
HATIMAYE
Rais Jakaya Kikwete ametimiza ahadi yake aliyoitoa Agosti mwaka jana katika
Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro, kwamba amekusudia kufuta ada ya shule za
sekondari nchi nzima.
Kwa
tangazo hilo, Bajeti ya mwisho ya uongozi wa Rais Kikwete itakayoanza
kujadiliwa Mei mwaka huu, itatakiwa kuwa na fungu la kulipa gharama ambazo
wananchi wamekuwa wakitoa kwa watoto wao wanaosoma elimu ya sekondari katika
shule za Serikali nchi nzima.
Kwa
sasa wazazi wamekuwa wakilipa Sh 20,000 kwa shule za kutwa na Sh 70,000 kwa
shule za bweni, ili watoto wao wapate elimu ya sekondari.
Ubora
Alisema
sera hiyo imezingatia stadi za msingi ambazo ni kuandika, kusoma na kuhesabu,
ili kuwezesha watoto kujengwa kwenye msingi mzuri na hata kwenye Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hilo limezingatiwa.
“Hata
kwenye mpango wa BRN tumelizungumza ili kuhakikisha inatolewa elimu bora.
Tusifanye mambo ya kuchekesha mtoto anafika madarasa ya juu hajui kuandika,
kusoma na kuhesabu. “Kuanzia sasa kama mtoto anafika darasa la pili, hajui
kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), ni bora asiende darasa la tatu…naamini
watoto wakiimarishwa katika stadi za KKK itaondoa matatizo haya,” alisema.
Tathimini
ya Msingi ya Taifa kwa ajili ya uwezo wa wanafunzi katika KKK, kwa wanafunzi wa
Darasa la Pili iliyofanyika mwaka jana, ilibaini kuwa asilimia 98 ya wanafunzi
wa Darasa la Pili nchini, walikuwa hawaelewi wanachokisoma.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema, tathimini hiyo
imefanywa kwa baraka za Wizara yake kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la
Marekani (USAID), ili kupata taarifa kuhusu hali halisi ilivyo ya wanafunzi wa
Tanzania kumudu stadi za KKK wanapofika Darasa la Pili.
Mafanikio
Mbali
na mafanikio ya kufikia uwezo wa kuanza kutoa elimu ya msingi na sekondari
bure, huku msisitizo ukiwekwa katika utoaji wa elimu bora, Rais Kikwete pia
ilitangaza mafanikio mengine katika sekta ya elimu ambayo yamefikiwa katika
uongozi wake wa miaka kumi.
Rais
Kikwete alisema sasa elimu imepewa kipaumbele katika sera na shughuli za
serikali, ndio maana Bajeti ya Elimu, ndio kubwa kuliko bajeti zote.
Alifafanua
kuwa mwaka 2005/06 bajeti hiyo ilikuwa Sh bilioni 6.7, wakati mwaka huu wa
fedha imepanda na kufikia Sh trilioni 3.1.
Hatua
hiyo ya kibajeti kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni ongezeko la mara tano ya Bajeti
ya mwaka 2005 sawa na asilimia 20 ya Bajeti ya Serikali ambayo inatengwa kwa
ajili ya elimu.
Katika
suala la mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema
imetoka Sh bilioni 56 kwa mwaka wa fedha 2005/06, hadi kufikia Sh bilioni 345
kwa mwaka huu wa fedha.
Aidha,
kwa mwaka jana, wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliongezeka
kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000.
Kwa
upande wa shule za msingi, alisema zimeongezeka kutoka 14,000 kwa mwaka 2005
hadi kufikia shule 16,343 kwa mwaka 2014, huku shule za sekondari zikiongezeka
kutoka 531 kwa mwaka 2005, hadi kufikia 4,576, mwaka 2014.
Idadi
wanafunzi wanaojiunga na sekondari, Rais Kikwete alisema imeongezeka kutoka
wanafunzi 524,325 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi milioni 1.8.
Rais
Kikwete alisema pia vyuo vya ufundi vimeongezeka kutoka vyuo 184 mwaka 2005 na
kufikia vyuo 744 kwa mwaka 2014, huku vyuo vikuu vikiongezeka kutoka vyuo vikuu
26 mwaka 2005 na kufikia vyuo vikuu 50 kwa mwaka 2014.
Alikumbusha
kuwa kama sio kuanzishwa kwa shule za kata, idadi ya wanafunzi pia
isingeongezeka.
“Hali
imebadilika, sasa wanafunzi wengi wanakwenda shule na vyuoni na suala la watoto
na vijana kupata fursa ya kusoma, sio tatizo katika sekta ya elimu, sasa
kinachotakiwa ni kuhakikisha inapatikana elimu bora kwa kuboresha mazingira ya
elimu,” alisema Rais Kikwete.
No comments:
Post a Comment