Ukisoma makala hii inaweza kukusaidia wewe au mtu unayemfahamu. Imeandikwa na Joyce Joliga
Kati
ya wanawake ambao wanaamini kuwa mafanikio hayaji bila kujituma kwa kufanya
kazi kwa bidii ni Salome Sanga (58).
Salome
ni mkazi wa Makambi katika Manispaa ya Songea na amekuwa akisifika kwa kufua
nguo kwenye nyumba za watu mbalimbali zaidi katika Kikosi cha Polisi FFU na
Kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania, Chandamali mkoani Ruvuma.
Mama
huyo wa watoto wanane ambaye awali aliolewa mwaka 1973 na Aloyce Haule ambaye
alizaa naye watoto watatu. Haule alifariki mwaka 1982 na miaka miwili baadaye,
alifunga ndoa na Vitalis Mumba ambaye alizaa naye watoto sita na mmoja kwa
bahati mbaya alifariki dunia hivyo kubaki akiwa na watoto wanane.
Anasema
walitengana na Vitalis kwa kuwa hali ya maisha ilikuwa ngumu na kila kukicha
alikuwa akipigwa na mumewe huyo ambaye hata hivyo alikuwa haihudumii familia
yake.
“Niliachana
naye nikaenda kupanga chumba na nilianza maisha ya upweke nikiwa na
wanangu wanne ambao tayari wameolewa wawili wako Dar es Salaam na wengine
wawili Majengo Songea na wengine wanaendesha maisha yao vijijini.
Anasema
anajivunia kufanya kazi hiyo ya kufua nguo katika nyumba za watu na wala
hajutii kufanya kazi hiyo na hatishwi na maneno ya watu ambao hudharau kazi za
watu.
Salome
anasema kupitia kazi hiyo, imemsaidia kufahamiana na watu mbalimbali pamoja na
kujipatia kipato kikubwa kinachomsaidia kuendesha familia yake bila msaada
kutoka kwa ndugu zake ama jamii inayomzunguka.
Kwa
sasa Salome anaishi na mama yake mzazi naye amezeeka pia ni mgonjwa hivyo
anamtegemea kwa mahitaji mbalimbali.
Anasema
anaifanya kazi hiyo kutokana na kukabiliwa na dhiki kubwa na amekuwa
akikabiliwa na matatizo mbalimbali, hivyo akaona njia ya kujikwamua ni
kujishughulisha na kazi hiyo ili kupata fedha za kujikimu na kulipa pango la
nyumba anayoishi.
“Unajua
sikwenda shule kwa kiasi kikubwa, nimeishia darasa la saba, sasa ninatumia
nguvu zangu kama mtaji,” anasema.
Anafafanua
zaidi kuwa, kazi ya kufua nguo za watu ni ngumu ingawa inampatia kipato
kikubwa.
“Nimekuwa
nikikutana na vikwazo pamoja na vitu mbalimbali ambavyo si vizuri
kuvizungumza lakini bado sijakata tama…Nimekuwa nikiendelea kufanya kazi hiyo
kwa uaminifu mkubwa niwaridhishe wateja wangu,” anasema.
Anasema
uaminifu ndiyo unaomfanya apate kazi nyingi na wakati mwingine anazikimbia kwa
kuwa zinamwelemea.
Anataja
changamoto nyingine kuwa ni baadhi ya wateja kutomlipa fedha zake kwa wakati ,
“Utakuta umefua na ukimaliza kazi mtu anakukopa lakini nashukuru Mungu
wengi ni waaminifu wamekuwa wakinilipa baada ya kumaliza kazi na wanaokuwa
hawana pesa siku hiyo, wakitoa ahadi siku inayofata wanaitekeleza,”
anasema.
Anasema:
“Changamoto nyingine ni kulipwa fedha kidogo tofauti na nguo za kufua na
utakuta kwenye hoteli kubwa nguo moja mtu analipa Sh1,000 hadi Sh2,500 lakini
kwa sisi tunaofua nyumbani wateja wetu wanatukadiria wenyewe utakuta anatoa
rundo la nguo na kukupatia Sh7,000 basi huwa tunaridhika na kupokea.
Kutokana
na kazi hiyo, anasema kwa siku anaweza kufua nguo katika nyumba tatu hadi nne
kutegemea na upatikanaji wa kazi anazopata.
“Ninaanza
kufua kwa kuanzia Sh3,000 hadi 15,000 na kujipatia pesa za kununua mahitaji
yangu madogo madogo…,” anasema.
Anasema
pamoja na kujishughulisha na kazi ya kufua nguo nyumbani pia
anajishughulisha na biashara ya uuzaji wa supu nyumbani kwake eneo la
Makambi na hata hivyo biashara hiyo haijampa faida kama inavyompatia
biashara ya kufua nguo nyumbani kwa watu.
Anasema
kwa sasa anajitahidi kuendelea kufanya kazi yake ya ufuaji nguo kwa ufanisi
mkubwa na anatamani siku moja kama Mungu atamjalia. Pia, akipata wafadhili wa
kumjengea nyumba ya kisasa ya kuishi na ataweka mashine za kisasa
za kufua nguo hivyo itamsaidia kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi ambao
watakuwa wanahitaji huduma yake badala ya kuendelea kuzunguka kwenye nyumba za
watu.