Muigizaji Angelina Jolie amelazimika kutoa mishipa ya
kupitisha mayai na vifuko vya mayai baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa
katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.
Muigizaji huyo maarufu wa Hollywood ameidokezea jarida la
New York Times, kuwa alilazimika kutoa uzazi wake juma lililopita katika
upasuaji wa dharura.
''Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa
daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya
kuambukizwa saratani'' alisema Bi Jolie
Habari hizi zimewashtua wafuasi na mashabiki wa totoshoo
huyo ambaye miaka miwli tu iliyopita alilazimika kukatwa matiti kwa sababu ya
tishio hilohilo la Saratani.
Aidha mamake muigizaji huyo nyota aliaga dunia kufuatia
hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.
''Sio jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu
linalohusu afya yangu'' alisema Jolie.
Jolie ambaye ni mkewe muigizaji nyota wa Holywood ctor
Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na
ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.
Wawili hao wanawatoto sita.
Mamake tayari aliaga dunia kutokana na Saratani
''Nilimpigia simu akiwa Ufaransa na akarejea nyumbani
mara moja ,lakini cha msingi ni kuwa ukikabiliwa na masaibu kama haya ya kiafya
na uwe una mtu anayeweza kukusaidia kwa kukuchangia mawazo mzigo unakuwa
mwepesi zaidi''
''Mamangu aligunduliwa kuwa na saratani akiwa na umri wa
miaka 49 hivi sasa nina miaka 39 ''
''Licha ya hayo hivi sasa nimeshakoma kuzaa kwa hivyo
ninatarajia mabadiliko mengi katika mwili wangu .Hivi sasa sina hamu ya kupata
watoto wengine ,alisema jolie.
“Nitastahimili kwa njia ileile ambayo nafikiri maelfu ya
wanawake wamepitia''
''Nilijiambia mwenyewe ni lazima nijikaze na kuwa na
nguvu maanake sikuwa na sababu ya kujifikiria mimi bila kuona watoto wangu
wakijuta na kusema looo! mamangu alikufa kutokana na saratani ya nyumba ya
uzazi'' alisema bi Jolie.
No comments:
Post a Comment