Baadhi yetu tunahamia nyumba mpya au chumba ambacho
hakina chochote ndani au hata kimepambwa tayari lakini unataka kubadilisha
muonekano. Sasa mtu anajiuliza hapa naanzia wapi kuki design. Napenda changamoto
hii kwa ajili
mimi ni homelover kwahivyo ninachojua kuhusu nyumba napenda
kuwashirikisha na wengine. Sasa ni kwa namna gani unaweza kuleta muonekano wa
kuvutia na kwa ladha yako chumbani. Hapa ni hatua tatu according to mimi:
Kwanza, fikiria vitu na rangi zinazokuvutia wewe binafsi.
Wengi wana rangi/vitu wanavyopendelea, kwa mfano, yupo
anayependelea wanyamawanyama, yupo wa mauamaua, yupo wa pundamilia, yupo wa
rangi plain labda brown, maroon, cream nk. Hapo ndipo pa kuanzia pale unapotaka kupamba
chumba.
Baada ya hapo amua ni nini kinaingia/kinabaki na ni nini
kinaondoka kati ya vitu unavyotaka viwepo hapo chumbani iwe ni sofa kitanda, zulia, sanaa ya ukutani nk.
Sasa anza kuviingiza kuvipanga kuanzia chini kwenda juu, maana yake ni kwamba
tuseme unataka kuweka carpet, usianze na meza kabla hujalitandika, ndio maana ya
kuanzia chini/sakafuni kwenda juu.
Ukishamaliza sakafu kifuatacho ni kuanza
kuingiza fenicha kubwa kwanza, kama ni sofa au kitanda au meza..zile ndogondogo
zitafuata baadae.
Halafu weka vitupio kama mito, maua na taa za
mezani.
Sasa hapa ni kama chumba kimeshakamilika na unaona vizuri kila kitu kivyokaa. Malizia kwa kutundika pazia, picha, fremu na sanaa zozote za ukutani za ladha yako. Kwa mawazo
yangu chumba hakijakamilika kupambwa kama ukuta ni mtupu.
Kwa dondoo nyingine ya muonekano wa nyumba tukutane kesho, hapahapa.
No comments:
Post a Comment