Madaktari wa upasuaji huko Cambridgeshire wamefanya
upandikizaji wa kwanza wa moyo barani Ulaya kwa kutumia moyo mwengine
uliosimama kufanya kazi.
Miyoyo hiyo hupatikana kutoka kwa watu waliokufa lakini
ambao miyoyo yao bado inafanya kazi.
Katika upasuaji huo,moyo huo ulitoka kwa mtu ambaye
mapafu yake na moyo wake ulikuwa haufanyi kazi.
Hospitali ya Papworth inasema kuwa mbinu hiyo huenda
ikaongeza idadi ya miyoyo inayopatikana kwa asilimia 25.
Mgonjwa aliyewekwa moyo mpya kwa jina Huseyin Ulucan,
mwenye umri wa miaka 60, kutoka London,alikabiliwa na shinikizo la moyo mwaka
2008.
Alisema:kabla ya upasuaji,sikuweza kutembea na nilichoka
sana,kwa hakika siku na maisha mazuri.
Lakini anasema kuwa amefurahishwa na kuimarika kwa afya
yake tangu upandikizaji huo.
Kwa sasa najisikia mwenye nguvu kila siku,na nimetembea
hadi haospitalini asubuhi hii bila tatizo.
Kumekuwa na visa 171 vya upandikizaji wa myoyo katika
kipindi cha miaka 12 iliopita nchini Uingereza.
Lakini mahitaji yanashinda miyoyo iliopo ,hivyobasi
wagonjwa wengine hungoja kwa miaka mitatu kupata kiungo kinachowafaa.
Wengi ya wagonjwa hao hufariki kabla ya kiungo kupatikana. CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment