WATANZANIA wameshauriwa kuachana na matumizi ya nguo
zilizotumika maarufu kama mitumba ambazo tayari baadhi zimeonekana kuwa na
madhara mbalimbali ya kiafya
yanayotokana na matumizi ya nguo hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa punguzo la asilimia
hamsini kwa nguo katika duka la Woolworths kwa ajili
ya sikukuu ya Pasaka
jijini Dar es Salaam jana, mkurugenzi wa duka hilo Joehans Bushiri alisema nguo
za mtumba si salama kwa matumizi kwa kuwa tayari zimeshatumika.
Alisema kuwa kwa kutambua hali hiyo tayari Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) limekuwa likitoa tahadhari kuhusiana na matumizi ya nguo
hizo ikiwa ni pamoja na kufanya operesheni mbalimbali za kuwakamata
wafanyabiashara.
“Tunawasihi Watanzania kuepukana na matumizi ya nguo za
mtumba kwani si salama kwa afya zao. Katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka
duka la Woolworths linatoa punguzo la asilimia hamsini ili kuwawezesha
Watanzania kupata nguo mpya na zenye ubora.Punguzo hili titadumu kwa wiki nne,”
alisema.
Bushiri alisema duka hilo ambalo ni moja kati ya maduka
makubwa ya nguo hapa nchini,litaendelea kuwahudumia wateja wake kwa kuwaletea
nguo nzuri kwa kutoa punguzo katika msimu huu wa Pasaka na kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa,duka hilo pia linatoa
nafasi kwa wateja kununua nguo kwa kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi
mitatu ili kuwawezesha wale wasio na fedha za kutosha kwa kulipa mara moja
kupata nguo nzuri pamoja na mahitaji mengine.
Kuhakikisha wateja wetu wanapata vitu bora kabisa,
vinavyoendana na wakati na kwa muda mwafaka, Woolworths imeweza kubadilisha
mfumo wa uletaji wa bidhaa nchini badala ya kutumia meli kama zamani sasa
inatumia usafiri wa ndege. Kabla ya hapo tulikuwa tunatumia muda wa mwezi mmoja
hadi miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa tunatumia muda wa wiki
mbili hadi tatu.
Bw. Bushiri pia akasisitiza kwamba anapenda
kuwahakikishia wateja wao kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote kama
zinazopatikana Afrika ya Kusini na kwa bei zinazofaa kabisa.
Alisema kuwa punguzo la bei limekuja kipindi kizuri
ambacho familia zinafanya manunuzi kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.
CHANZO: MAJIRA
No comments:
Post a Comment