Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi
umegundua kwamba masomo ya nyumbani apewayo mwanafunzi baada ya saa za shule
inashauriwa aifanye si zaidi ya dakika sitini sawa na saa moja tu ili aifanye
kwa ufanisi mkubwa.
Na endapo itamchukua dakika tisini kuyafanya masomo hayo
ya nyumbani matokeo yake hayatakuwa mazuri, utafiti umebaini. Utafiti mpya nao
umeng’amua kwamba watoto hawapaswi kusaidiwa na walezi ama wazazi wao kufanya
masomo hayo ya nyumbani.
Nao wanafunzi mara zote wamekuwa wakilalama kuwa masomo
ya nyumbani yakiwa mengi ni mbaya kwao, watafiti baada ya tafiti zao
wanakubaliana na malalmiko ya wanafunzi.
Kwa watoto walio katika ukuaji na wanaojisomea kwa juhudi
ili kupata matokeo mazuri,waalimu hawapaswi kuandaa kazi ngumu kwa wanafunzi
hao,lakini kazi ikiwa katika daraja ya kati humfanya mwanafunzi kuelewa zaidi.
Dr Javier Suarez-Alvarez anasema kwamba utafiti wao
umeainisha kwamba hakuna sababu ya mwalimu kumlimbikizia mazoezi
mwanafunzi,lakini ni muhimu mazoezi ya nyumbani yawe katika mpangilio ufaao kwa
lengo la kumfanya mwanafunzi awe na mazoea ya kujifunza hata baada ya masomo ya
darasani na hii itamsaidia kupenda,uhuru na tabia ya kujisomea yeye binafsi
hata baada ya maisha ya shule .
Utafiti wa hivi karibuni,uliofanywa na chuo cha Stanford
umegundua kuwa mwanafunzi afanyapo masomo ya nyumbani kwa zaidi ya saa tatu kwa
usiku mmoja humfanya mwanafunzi augue.
Utafiti huo uliwahusisha wanafunzi elfu nne na mia tatu
kwa wanafunzi kumi bora wa shule za serikali hata za binafsi katika jimbo la
Califonia,na kuweka bayana kuwa masomo mengi ya ziada humletea mwanafunzi
msongo wa mawazo na kuleta matatizo mengine ya kiafya.
Moja ya matatizo yanayotajwa ni msongo wa mawazo, lakini
pia masomo ya nyumbani yakiwa lukuki humletea mwanafunzi vidonda vya
tumbo,kukosa usingizi ama kupata usingizi wa mang’amung’amu,kupungua uzito wa
mwili ,na kuwa mchovu muda mwingi,huu ni utafiti alioufanya Denise Pope.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment