WADAU wa matumizi ya mtandao wametoa tamko la kuliomba
Bunge lisipitishe Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao kuwa sheria, kwa kuwa
unaingilia uhuru wa mawasiliano kwa wananchi.
Muswada huo unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi
ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu
wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki.
Wadau hao, muswada huo haukuwekwa wazi hadi tarehe 29
Machi na ratiba inaonesha muswada huo utapitishwa chini ya hati ya dharura
tarehe 31 Machi, hivyo wananchi hawajapata nafasi ya kupitia kwa kina na kutoa
maoni yao kuhusu muswada huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari
jana na wadau hao, iliyowakilisha wananchi wanaotumia mitandao muswada huo
usipitishwe ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi kushiriki kikamilifu katika
kuandika sheria hiyo muhimu.
“Sisi wadau tunaowakilisha wananchi wanaotumia mtandao
tunaomba Bunge lisipitishe Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 kuwa
sheria,” ilisema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Shirika la
Sikika, Erinei Kiria.
Wadau hao walisema kuwa kutokana na umuhimu wa Muswada
huo unaolenga kudhibiti uhalifu wa mitandao, lakini kwa namna ulivyo unaingilia
uhuru wa mawasiliano.
“Muswada huu usipitishwe ili kutoa nafasi kwa wananchi
wengi kushiriki kikamilifu katika kuandika sheria hii muhimu,”ilisema taarifa
hiyo.
Hata hivyo Muswada huo unalenga na kuhusisha kudhibiti
mawasiliano ya wananchi wenyewe kwa wenyewe suala ambalo linaweza kupingana na
katiba ya nchi sheria zilizopo na haki za binadamu za umoja wa mataifa.
Wiki iliyopita Bunge lilipitisha sheria ya Takwimu ambao
unawabana wanahabari watakaoandika takwimu ambazo hazijaruhusiwa kutolewa na
serikali wako hatarini kulipishwa faini ya Sh milioni 10 au kifungo kifungo
kisichopungua mwaka miwili jela.
Mapendekezo ya adhabu hizo yako katika Muswada wa Sheria
ya Takwimu ya mwaka 2013, ambayo ni miongoni mwa miswada miwili inayowasilishwa
ndani ya Bunge.
Kwa mujibu wa ibara ya 20(1) ya sheria hiyo, muswada
unataja taasisi tatu ambazo ndizo kisheria zitakuwa zikiruhusiwa kutoa au
kuchapisha takwimu rasmi na si vinginevyo. Taasisi hizo ni Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS), Taasisi za Serikali na Wakala wa Serikali.
Kwa lugha rahisi, muswada unazuia waandishi na vyombo
vyao kuacha kuandika habari za takwimu ambazo hazijatolewa rasmi na adhabu zake
zinaanzia kifungo kisichopungua mwaka mmoja na faini ya kuanzia shilingi
milioni tano na kuendelea.
“Mtu yeyote, kwa kujifanya anatimiza majukumu yake, iwapo
anapata au anaomba kupatiwa taarifa ambayo haijaidhinishwa kuipata na
kuichapisha au kuisambaza atakuwa amefanya kosa ambalo adhabu yake ni kifungo
kisichopungua miezi 12 au fani isiyopungua shilingi milioni mbili au vyote kwa
pamoja,” inasema ibara ya 37 (d) cha muswada huo.
Muswada huo unaainisha wazi kwamba takwimu rasmi ni zile
ambazo zimetolewa na kuidhinishwa na taasisi zilizoelezwa kwenye ibara hiyo ya
20 na ndizo pekee zinazoweza kutumika kama ushahidi kwenye kesi.
CHANZO MTANZANIA
No comments:
Post a Comment