TCRA
izimulike blogs ‘Uchwara’ na kuzichukulia hatua kali
Soma makala hii kutoka Dewji Blog imeandikwa Na Andrew Chale wa Modewji blog
“Screen shot”
ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara kuhusiana na
taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika
habari za uongo, matusi
Miongoni mwa mambo
ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali
ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine
mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo
wanayoyatumia vibaya.
Kupitia BLOG,
mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama
kufanyia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo
halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa
wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni mwa
mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote
anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha
BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari
zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazo si za kweli.
Tunaamini wapo watu
wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa
si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na
zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii,
kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata
kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu
wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao
kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye
blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha
kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni
haki?, tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama
kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa
Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority
(TCRA), ( https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama
mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke huko nyuma
kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo
walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka
picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi
wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka
shuka wakati mambo yamekua si mambo.
Hivyo ni wakati
sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo
kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao huu unaamini
kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya
kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni
pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye
miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi
huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?”
wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanapokutana na
habari kwenye hizo blog uchwara.
Wadau waliochangia
mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha…. hili ndiyo tatizo
kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed
journalist… UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu
chefu… full of attention-seeking sensationalism… utakuta heading: HATARI, Vilio
na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog
zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo wachangiaji
wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili
kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
Modewji blog tunaamini
pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani
kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA
AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu likilipuka
tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo,
mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “
#Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.
Tuandikie maoni yako
kupitia kwenye mtandao huu hapo chini ama kupitia simu 0719076376 au 0714940992.
Dewji Blog
No comments:
Post a Comment