Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la
Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa
taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika
Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa
raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti
wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea
kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria,
kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi.
Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni.
Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani
bila mafanikio.
Buhari alimshinda rais anayeondoka Goodluck Jonathan
katika uchaguzi ulioshuhudia ushindani mkubwa
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi
mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na
ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu
ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria
sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha,
miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri,
kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira.
Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado
unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment