MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, Josephine Mushumbusi jana ametoa maelezo
yake katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kuhusu tuhuma za kutaka
kuuawa kwa katibu huyo.
Akiwa amefuatana na Dk Slaa, Mushumbusi alifika
kitu kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kutoa maelezo kwa saa mbili.
“Nimekuja kutoa maelezo yangu, sikuwa na mengi
ya kusema zaidi ya kile ninachokifahamu,” alisema na kusema wakati mwito
ulipotolewa kwenda kutoa ushahidi, hakuwa nchini.
Dk Slaa alisema, Mushumbusi amemaliza kazi yake
ya kutoa maelezo na taarifa waliyoipata ni kuwa mashahidi wamemaliza kutoa
ushahidi wao, hivyo wanasubiri hatua zaidi.
“Mama alikuwa anatoa ushahidi na amemaliza kazi
yake, lakini ikumbukwe huyu siyo mtuhumiwa hajaja kuhojiwa ila ni shahidi, kwa
sababu ukisema kuhojiwa ina maana ni mtuhumiwa,” alisema Dk Slaa.
Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa madai kwamba
aliyekuwa mlinzi wa Dk Slaa, Khalid Kagenzi, alitaka kumwekea sumu Katibu Mkuu
huyo.
Hata hivyo, Kova alipoulizwa kuhusu kuwepo
Mushumbusi kituoni hapo kutoa maelezo yake, alisema hana taarifa yoyote na hata
kama akiwepo, ni hali ya kawaida.
Alisema ingekuwa ni jambo tofauti au kubwa angepata
taarifa lakini kitendo cha mtu yeyote kuitwa kutoa maelezo ni cha kawaida.
CHANZO: HABARILEO
No comments:
Post a Comment