Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali
Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na kumuondoa rais aliyeko Goodluck
Jonathan mamlakani.
Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan
amekwisha mpigia simu mpinzani wake Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi
huo wa kihistoria.
Hii ndiyo mara kwanza katika historia ya taifa hilo kwa
rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.
Goodluck amekiri kushindwa katika uchaguzi huo
ulioshuhudia ushindani mkali
Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana
kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya
kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.
Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume
ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao
wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile
kimajimbo .
Wanigeria wengi wamefurahi kushiriki uchaguzi uliomtoa
mamlakani raisl aliyekuwa hatekelezi wajibu wake
Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye wameweza
kuing'oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake kikamilifu.
Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume
hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya
mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.
BBC
No comments:
Post a Comment