Rubani Andreas Lubitz |
Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka
katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege
hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.
Kiongozi wa mashtaka katika mji wa
Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika
kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa
ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.
Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi
huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani
ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga yowe kabla ya
kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
Mlima wa Alps ambapo ndege ya abiria ya Germanywings
ilianguka
Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka
28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka
alisema.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona
kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja
na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua
udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga
nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment