Monday, March 23, 2015

MTOTO AFUNGIWA NDANI NYUMBANI KWAO HUKO TEXAS.......POLISI ALIYEMWOKOA ASEMA AMEFANYA KAZI MIAKA 30 NA HAJAWAHI KUKUTANA NA TUKIO LA NAMNA HIYO

Mtoto aliyekuwa akifunguwa ndani
Picha ya kushtusha imeachiliwa kwa ulimwengu hivi karibuni picha inayomuonesha mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano aliye kondeana ,aliyetelekezwa katika sehemu ya chini ya nyumba yao ,aliyefungiwa na kuachwa afe njaa na familia yake.
Tammi Bleimeyer,mwenye umri wa miaka 33,na mumewe Bradley,mwenye miaka 24, wameshtakiwa kwa kosa la kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa katika hali dhoofu katika majira ya baridi ,kitongoji cha Harris, huko Texas.

Askari aliye fanikisha kupatikana kwa mtoto huyo Mark Herman,amesema kwamba amefanya kazi ya polisi katika kipindi cha miaka thelathini lakini hajawahi kushuhudia tukio la namna hii.

Askari huyo anasema wamemkuta mtoto huyo katika hali mbaya ana njaa kali,amekondeana,amevilia damu mwilini kama aliyekuwa akipigwa ama kupitia mateso makali na ngozi yake ilionekana kama imeachana na mifupa ,ilikuwa ni hali ya kutisha sana kumwona mtoto katika hali hiyo.

Bradley alikuwa akibishana na mtoto huyo wa kambo mwenye umri wa miaka kumi na sita aliyekuwa akiwataka wazazi wa mtoto huyo kuacha kumfungia mtoto wao katika chumba cha chini ya ardhini nyumbani mwao .

Na polisi walipofika nyumbani hapo waligundua chumba kidogoo,chini ya nyumba hiyo kikiwa kimefungwa na godoro tu ndani yake na mtoto aliyeketi juu ya godoro ,ingawa mama wa kambo wa mtoto huyo alimtorosha baada ya kujua kwamba polisi wanamfuatilia, na kumkuta katika chumba cha hoteli na kumfuatilia hatimaye kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa matibabu.

Ingawa mpaka mtoto huyo anafikishwa hospitalini, sababu za kufungiwa kwa mtoto huyo hazikufahamika mara moja ,na wazazi wa mtoto huyo wamekataa kuzungumzia tukio hilo .


Baba wa mtoto huyo anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na mtoto wake bado amesalia hospitalini kwa matibabu zaidi katika hospitali ya watoto iliyoko mjini Texas . Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment