Madaktari wanasema kuwa wazazi wengi hawajui madhara ya
afya kwa watoto walionenepa kupita kiasi.
Katika utafiti uliowajumuisha zaidi ya familia 2,976
nchini Uingereza ni wazazi 4 pekee waliokuwa na shauku kuwa mtoto wao alikuwa
amenenepa kupita kiasi.
Madaktari wenyewe walikuwa wamewatambua watoto 369 kati yao
waliokuwa na kiwango cha juu cha mafuta mwilini.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa watoto walionenepa kupita
kiasi sasa wamekuwa kawaida tu majumbani.
Watafiti hao wanaonya kuwa hili ni janga kwa afya ya
jamii.
Asilimia 31% ya wazazi hawajui kutambua dalili za mtoto
aliyenenepa kupita kiasi.
Aidha utafiti huo ulielezea kuwa takriban mtoto mmoja
kati ya watano ambao wanaumri wa miaka 6 tayari wanauzito unaozidi kadri kwa
asilimia 14%.
Kundi hilo la watafiti kutoka taasisi ya usafi ya
Uingereza ''London School of Hygiene and Tropical Medicine'' lilizitembela familia
3,000 na kuwahoji iwapo watoto wao walikuwa ni wanene kupita kiasi wastani ama
wembamba?
majibu yao yaliwaduwaza.
Takriban thuluthi moja 31% ya wazazi walidunisha uzani wa
watoto wao.
Proffesa Russell Viner, wa chuo cha Afya ya Watoto
aliiambia BBC kuwa wazazi wa kisasa wanamajukumu wengi na hivyo watoto wao
hutunzwa na vijakazi asilimia kubwa ya muda ambao wazazi wako makazini mwao.
''Hili ni janga ambalo linatokota ,madhara yake
yataonekana siku za usoni katika njia ya maradhi mengi tu yanayohusiani na
unene'' alisema Professa Viner.
Kwa mujibu wa Daktari Dame Sally Davies, ''Afya ya watoto
kwa sasa imehujumiwa na dhana kuwa japo mtu ni mnene jamii haitambagua kwani
watu wengi duniani ni wanene''
"Nafikiri kwamba itatubidi tuwaelimishe wazazi
kuhusiana na maswala ya afya ya watoto wao na pia kuwaeleza kuwa wanapaswa
kufuatilia kwa karibu unene au sio wa watoto wao''
Anapendekeza kuwa sheria madhubuti zinapaswa kutungwa
ili kuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi.
No comments:
Post a Comment