Uchunguzi wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha
kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa mmoja wa marubani
wa ndege hiyo alikuwa amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo
ilipoanguka.
Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa ameondoka kufanya
nini lakini sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka ufunguliwe mlango.
Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la New York
Times.
Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema kwa kinywa
wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.
''hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali hiyo ''
''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati majuzi tu wala
haikuwa na hitilafu yeyote''.
nini kilitokea? swali halina jibu,kisanduku cheusi
kimeharibika
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata
kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya
shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.
Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku
kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo .
Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko
upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa
katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.
David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege
,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini
kilichotokea .
pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi
wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo
ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu,
na hatua walizochukua kunusuru janga hilo.
Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria
na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege?
Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini
walichokiacha na mambo kama hayo.
Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili
tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten
Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika
dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa
isiyoeleweka.
Niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii
nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa,bado hainiingii
akilini juu ya kile kilichotokea jana.
Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege
yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo ,bado
hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali
nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia
mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa,kuhusika
katika ajali mbaya kiasi kile .
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment