Mtandao wa kuwakutanisha wapendanao na unaowalenga watu
walio katika ndoa nchini Ufaransa umeshtumiwa kwa kuvunja sheria.
Mahakama moja nchini Ufaransa sasa inatarajiwa
kuamua
iwapo mtandao huo unawafanya wanandoa kufanya udanganyifu.
Je, inakubalika kuwepo kwa mtandao unaokuza
uashereti,ambapo uaminifu katika ndoa umewekwa katika sheria za taifa hilo?
Hilo ni swali linalokabili kampuni ya Gleeden ambayo
inasifika kwamba ndio kampuni inayowapatia wanawake raha za ziada za nje ya
ndoa.
Muungano wa familia za kikatoliki ambao umekasirishwa na
matangazo ya kampuni hayo umefungua kesi dhidi yake likitaka kujua uhalali wa
mtandao huo.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment