Mwanamume mmoja nchini Saudia amempa talaka mkewe
kutokana na ujumbe wake katika mtandao wa WhatsApp.
Kulingana na gazeti moja la kiarabu Al Hayat, mwanamume
huyo amedai kwamba mkewe aliandika ujumbe unaosema ''naomba kuwa na subra ya
kutosha ili kuweza kuishi na wewe''.
''Nilimpigia mmoja ya ndugu zangu kumuuliza iwapo ujumbe
ule ulikuwa unanilenga mimi'', alisema mwanamume huyo.Watu wa Familia yangu
walithibitisha hilo na nilisikia aibu kubwa kwamba mabibi za marafiki zangu
pamoja na watu wa familia yangu wanaona ninaaibishwa.Hata sielewi alikuwa
akimaanisha nini''.
Amesema kuwa ndo yake ilikuwa taabani na kwamba kitendo
hicho hakikustahili kufanyika.Si mara ya kwanza amenichafulia jina katika
mtandao wa kijamii.Niliamua kumpa talaka kabla ya kuyatamgaza maisha yangu
katika mitandao ya kijamii.'',
Khalid Al Habibi ,naibu mkurugenzi wa kituo cha kijamii
kinachojihusisha na watoto mayatima anasema kuwa mitandao ya kijamii ni chanzo
kikuu cha talaka.
No comments:
Post a Comment