Wanawake wote walioamua kupamba sehemu zao za siri kwa
kuzitoboa wanachukuliwa kuwa wamepitia ukatili wa kijinsia ama wamekeketwa kitengo
cha afya kimetanabahisha hayo.
Hata kama mtu huyo amefikia umri wa utu uzima na
ameyafanya hayo kwa ridhaa yake,bado atahesabika kuwa alipitia ukatili wenye
madhara kwa afya yake,na inapaswa kuchukua tahadhari kubwa kuweka kumbu kumbu
za watu walio toboa sehemu zao za siri.
Lakini kujichora mwilini maarufu kama Tattoo ama kutoboa
sehemu za siri ama mwilini,kumepingwa na taasisi ya utoboaji na uchoraji tattoo
mwilini kwamba hakuna uhusiano wowote na ukeketaji.
Na kueleza kuwa vitu hivyo viwili havichangamani
kulinganisha na kutoboa sehemu za mwili wa mwanadamu,na taasisi hiyo
wanachukulia suala la kutoboa mwili kama jambo la kaiwada na la ridhaa anasema
msemaji wa taasisi hiyo Marcus Henderson.
Zaidi ya matukio ya ukeketaji yapatayo mia mbili
yaliyochunguzwa na polisi wa kimataifa miaka mitano iliyopita,na inashauriwa kama
kuna mtu mmoja ana mashaka na suala ya ukeketaji wataarifu polisi.
Watoboaji makini huwa hawataki kuumiza wateja wao na huwa
hawataki kuonesha tundu za kazi zao na hawako tayari kumtoboa mtu aliye chini
ya umri wa miaka kumi na nane,anaeleza Mr Henderson.
Mtoboaji maarufu kutoka mjini London ambaye ametaka
ahifadhiwe jina lake, amesema kwamba wateja walio wengi huwa wanataka
kutobolewa sehemu zao za siri zisilingane na ukeketaji.
Sihusiki na ukeketaji,nadhani utoboaji ni zaidi ya pambo
mwilini ama uvumbuzi mpya wa kihisia zaidi.
Mtoboaji huyu anadai kwamba huwa anaitekeleza kazi yake
kwa ufanisi mkubwa,kwanza huangalia picha kwa umakini mkubwa kabla hajamtoboa
mtu, na kamwe hawezi kumtoboa mtu aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane.
Na wateja wake walio wengi ni wanawake na hutoboa sehemu
ya siri hasa kwenye pezi la sehemu ya kati ya maungo ya mwanamke.
Ingawa mtoboaji huyu mashuhuri mwanzoni alikuwa hakubali
kutoboa sehemu za siri za wanawake,na hii ni kutokana na maungo hao yalivyo na
hatari inayowakabili kupitia utaratibu huo.
Naye msemaji kutoka kitengo cha afya ambaye ni mwanamke
anasema kwamba,kuna changamoto kwa baadhi ya maeneo wanawake watu wazima
hutobolewa sehemu zao za siri kilazima na maeneo mengine wasichana hulazimishwa
kutobolewa.
Idadi ya wanawake waliokeketwa nchini Uingereza inatajwa
kufikia laki moja na elfu sabini,na zaidi ya wanawake na wasichana elfu mbili
na mia sita wamehudumiwa na kitabibu tangu September na kati ya hao ,mia nne
tisini na tisa walitambuliwa January mwaka huu pekee.
Nayo serikali ya Uingereza imesema kwamba haina mpango wa
kuifanyia marekebisho sheria ya mwaka 2003 kuingiza suala la kufanya upasuaji
kwa masuala ya urembo kwenye sehemu za siri.
Kamati teule ya wabunge katika taarifa yake imesema
kwamba sheria hiyo haina budi kubadilishwa ili kuweka wazi juu ya taratibu hizo
kuwa ni kinyume cha sheria na zaidi ni kosa la jinai kama zitafanywa kwa
msichana wa chini ya miaka kumi na nane isipokuwa kwa sababu ya afya ya akili
au kimwili.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment