Ndege moja ya shirika la ndege la British Airways
imelazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea kwa choo.
Ndege hiyo ya BA ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza
kutoka Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua saa saba.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo bwana Abhishek
Sachdev, aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa ''Amini
usiamini ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya
wahudumu
kugundua kuwa harufu mbaya inatokea kwenye choo ya ndege
hiyo.''
Yamkini rubani wa ndege hiyo aliwaita msimamizi wa
wahudumu wa ndege hiyo ndipo tukang'amua kuwa kulikuwa na tashwishi katika
safari yetu''Sachdev alinukuliwa na gazeti moja.
''mara tukaelezwa na rubani kuwa harufu mbaya ndani ya
ndege hiyo inatokea kwenye choo kichafu na kuwa ilikuwa ni ya kinyezi''
''Kufikia wakati huo ilikuwa ni takriban nusu saa tangu
tupae angani kwa hivyo tukalazimika kurejea Dubai''
''Ajabu ni kuwa hakukuwa na ndege mbadala ya kuturejesha
London kwa hivyo ikatubidi kusubiri kwa zaidi ya saa 15 .
hata hivyo walitupeleka hotelini tukapumzika usiku
kucha''
Mwakilishi wa ndege hiyo Greg James, Sarah, aliiambia
Radio 1 kuwa hilo halikuwa swala la kufanyiwa utani kwani ukiwa ndani ya ndege
ni tishio kubwa kwa afya ya rubani na abiria kwa jumla.
''Ndani ya ndege huwa kunautupu wa hewa kwa hivyo asili
mia 50 ya hewa inayotumika ni ileile kwa hivyo harufu mbaya ingeathiri vibaya
afya ya abiria ndio sababu ndege hiyo haikuwa na budi ila kurejea
iliisafishwe''.
Hata hivyo shirika hilo la ndege liliomba msamaha kwa
usumbufu wowote kwa abiria wake walioathirika siku hiyo.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment