Ikiwa imepita miezi isiyopungua mitano baada ya msanii
Ney wa Mitego kumpata mwanae wa tatu anayefahamika kwa jina Curtis, staa huyo
ametoa kauli nzito kuwa kwa sasa hana mahusiano wala mapenzi yoyote kwa wamama wa
watoto wake.
Kauli hiyo iliyoonekana kuwashangaza mashabiki wa msanii
ambapo Ney pia amesema kuwa mapenzi
yake yote kwa sasa yapo kwa wanawe tu.
Ney ambaye kwa sasa pia kuna tetesi za kuwa anatarajia
mtoto mwingine, tetesi ambazo amezikanusha kiutata, amesema kuwa kwa sasa hahitaji kabisa mwanamke, na watoto wake pekee ndio wanampa nguvu na
kumhamasisha kujituma kila siku.
Chanzo: EATV
No comments:
Post a Comment