Kiongozi wa Chechnya, Ramzan Kadyrov |
Nimekutana na hii habari nikafurahi. Wanawake hao wamenyimwa kutumia whatsapp kutokana na binti wa miaka 17 aliyelazimishwa kuolewa..nilipost hii habari huko nyuma tatizo sijajua kuweka link ningeweka hapa..
Kiongozi wa Chechnya Ramzan Kadyrov amewataka wanaume
kuwazuia wake zao kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp baada ya mada ya ndoa
ya lazima kusambaa katika ujumbe mfupi wa simu.
Kadyrov
amekaririwa akisema "wafungieni ndani, msiwaache wakatoka nje, kwa hiyo
hawatatuma chochote,"
Bwana
Kadyrov mapema aliunga mkono ndoa ya afisa wa Polisi kumwoa msichana wa miaka
17, japokuwa alikuwa tayari
ameolewa, katika tukio la ukiukaji wa sheria za
Urusi.
Mnadhimu
wake wa kijeshi tangu wakati huo alipendekeza kuhalalisha ndoa ya zaidi ya mke
mmoja nchini Chechnya.
Bwana
Kadyrov, kiongozi wa kimila na mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi, Vladimir
Putin, katika miaka ya karibuni alipiga marufuku kuwachukua kwa nguvu wanawake
kwa ajili ya kufunga nao ndoa za umri mdogo.
Pia
anafikiriwa kuwa anapendelea ndoa za wake wengi. Msaidizi wake mkuu Magomed
Daudov anasema: "hiyo yote inaendana na Sharia. Lakini kama mwanaume
anaweza kuhudumia zaidi ya mke mmoja, kwa nini asioe wengi?" Watu wengi
katika jamhuri ya ya Urusi ya Chechnya, ni Waislamu.
BBC
No comments:
Post a Comment