WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha
wahariri wakuu wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao
mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika mkutano huo kwa ufupi
Lowassa amesema yafuatayo;
1: Amesema hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio
sababu hata
kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa
cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa
bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika
kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda
mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi
hii.
2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga
mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi,
Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni
waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga
Elibariki Kingu. Pia aliekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki
ametangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya
kampeni ya Lowassa. Amehoji kwani akina karamagi wana tatizo gani na kwani wao
sio binadamu?
3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo
kwanza cha serikali ya JK. Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na
kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza.
4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na
ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara
yotote.
5. Anasema hatahama CCM na asiemtaka yeye CCM ndie
aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.
6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika
siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.
7. Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na
kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali
wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.
Hayo ni kwa ufupi. Wahariri wakuu katika media zote
kupitia Jukwaa la Wahariri walikuwepo, na Absalom Kibanda na Nevil Meena ndio
walikuwa waratibu wakuu wa mkutano huu.
CHANZO: JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment