Mahakama moja nchini Misri imetoa amri ya kunyongwa kwa
aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi.
Mahakama hiyo ilimpata na hatia aliyekuwa rais wa Misri
Mohammed Morsi kufuatia kuvunjwa kwa magereza mwaka wa 2011.
Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye
alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa
waandamanaji waliopinga utawala wake.
Morsi aling'olewa mamlakani na jeshi mwezi Julai mwaka wa
2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake.
Kuanzia hapo chama chake cha the Muslim Brotherhood
kimepigwa marufuku huku mamia ya maelfu ya wafuasi wake kukamatwa na vyombo vya
dola.
Kufuatia uamuzi huo wa kifo , sasa kauli nzima na ruhusa
itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye sasa
ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi ataonja mauti au la .
Sheria za nchi hiyo hata hivyo zinamruhusu Morsi kukata
rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.
Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kuwa mashtaka
dhidi yake yamechochewa na uhasma wa kisiasa baina yake na uongozi ulioko sasa.
Morsi amekataa katakata uhalali wa mahakama iliopo sasa.
Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza
kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.
Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano
baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa ofisini.
BBC
No comments:
Post a Comment