BALOZI wa kudumu wa Umoja wa Afrika (AU), huko Marekani,
Mtanzania Amina Salum Ali, (Pichani) akitangaza jana Jumatano Mei 20, 2015, pale
kwenye mgahawa wa Hadees jirani na askari monument, kuwania urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25,
2015.
Balozi Amina ametangaza uamuzi wake huo mapema leo hapa
hapa jijini Dar es Salaam.Itakumbukwa ya kuwa Balozi Amina ambaye alidumu kwa
muda mrefu kama waziri kwenye serikali ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin
Amour Juma, almaarufu kama (Komandoo), aliwahi kutupa karata yake kuwania urais
wa Zanzibar, kabla ya kujitoa.
Huyu anakuwa mwana mama wa kwanza kwenye historia ya
chama cha Mapinduzi CCM, kutangaza kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
VIJIMAMBO
No comments:
Post a Comment