Mchezajii wa kilabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor
amepewa mapumziko kwa mara ya pili msimu huu lakini hatma yake katika kilabu ya
Spurs haijulikani.
Mchezaji huyo wa taifa la Togo mwenye umri wa miaka 31
ameandika kuhusu matatizo ya famili yake katika mtandao wa facebook na kusema
kuwa alikuwa ameamua kujiuua.
Atakosa mechi ya siku ya jumapili kati ya kilabu yake na
Everton mbali na ziara ya Kuala Lumpur na baadaye nchini Sidney.
''Tumempa muda wa kusuluhisha mzozo na familia
yake'',alisema kocha wa kilabu hiyo Mauricio Pochettino.Ni miasha yakje ya
kibinafsi .Niliongea naye mapema wiki hii,ni hali ngumu kwake''.
Adebayor alijiunga na klabu ya Spurs mwaka 2011 kutoka
Manchester City kupitia mkopo kabla ya mabao 18 aliyofunga akiwa na Hotspurs
kumwezesha kupewa kandarasi ya kudumu.
BBC
No comments:
Post a Comment